Biblia inasema nini kuhusu kusema kweli
Vifungu 6 kuhusu kusema kweli, vimetafsiriwa kutoka Kiebrania na Kigiriki.
Vifungu hivi vilichaguliwa kwa msaada wa AI na bado havijakaguliwa na mkaguzi aliyetajwa.
Mithali 12:22
BWANA huichukia midomo ya uongo, bali watu waaminifu ni furaha Yake.
Waefeso 4:25
Basi sasa kwa kuwa mmeuvua uongo, kila mmoja wenu amwambie jirani yake kweli, kwa maana sisi kwa sisi ni viungo.
Wakolosai 3:9–10
Msiseme uongo ninyi kwa ninyi. Mmeuvua utu wa zamani pamoja na mienendo yake, mkauvaa utu mpya, ambao unafanywa upya na kukua katika ujuzi, kwa sura ya Muumba wake.
Kutoka 20:16
Usitoe ushahidi wa uongo dhidi ya jirani yako.
Mithali 19:5
Shahidi wa uongo hataepuka adhabu, naye anayebubujika uongo hatanusurika.
Zekaria 8:16
Haya ndiyo mambo mnayopaswa kufanya: Ambianeni ukweli ninyi kwa ninyi. Katika mahakama zenu toeni hukumu zilizo za kweli na za haki, zinazoleta amani.
Mada za Biblia
Wema · Msamaha · Hasira · Kuwaheshimu wazazi · Umoja · Uchungu · Ibada ya sanamu · Amani · Watoto · Hekima