Biblia inasema nini kuhusu kuwaheshimu wazazi
Vifungu 6 kuhusu kuwaheshimu wazazi, vimetafsiriwa kutoka Kiebrania na Kigiriki.
Vifungu hivi vilichaguliwa kwa msaada wa AI na bado havijakaguliwa na mkaguzi aliyetajwa.
Kutoka 20:12
Waheshimu baba yako na mama yako. Ndipo utaishi muda mrefu katika nchi ambayo BWANA Mungu wako atakupa.
Waefeso 6:1–3
Watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, kwa sababu hili ni jambo la haki. “Waheshimu baba yako na mama yako.” Hii ndiyo amri ya kwanza iliyoambatana na ahadi: “ili mambo yakuendee vizuri, na ufurahie maisha marefu duniani.”
Wakolosai 3:20
Ninyi watoto, fanyeni yote wazazi wenu wanayowaambia, kwa maana hilo ndilo linalopendeza katika Bwana.
Mithali 1:8–9
Mwanangu, sikiliza baba yako anapokuonya, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. Kwa maana yatakuwa shada zuri kichwani pako na mapambo yanayoning’inia shingoni mwako.
Mithali 23:22
Msikilize baba aliyekupa uhai, wala usimdharau mama yako atakapozeeka.
Mambo ya Walawi 19:3
Kila mmoja wenu amche mama yake na baba yake, na mzishike Sabato Zangu. Mimi ni BWANA Mungu wenu.
Mada za Biblia
Watoto · Akina mama · Kusema kweli · Malezi ya watoto · Akina baba · Ibada ya sanamu · Msamaha · Amani · Nguvu · Hasira