Biblia inasema nini kuhusu uaminifu wa Mungu
Vifungu 6 kuhusu uaminifu wa Mungu, vimetafsiriwa kutoka Kiebrania na Kigiriki.
Vifungu hivi vilichaguliwa kwa msaada wa AI na bado havijakaguliwa na mkaguzi aliyetajwa.
Maombolezo 3:22–23
Ni kwa upendo usiokoma wa BWANA kwamba hatujafutiliwa mbali, kwa maana huruma Zake hazijapungua. Zinafanywa upya kila asubuhi; jinsi ulivyo mkuu uaminifu Wako!
Kumbukumbu la Torati 7:9
Basi tambua kwamba BWANA Mungu wako ndiye Mungu wa kweli, Mungu mwaminifu. Hulishika agano Lake na upendo Wake wa uaminifu kwa vizazi elfu pamoja na wale wanaompenda na kuzishika amri Zake,
2 Timotheo 2:13
Tusipokuwa waaminifu, Yeye hubaki mwaminifu, kwa maana hawezi kujikana Mwenyewe.
1 Wakorintho 10:13
Jaribu lililowapata si jingine ila lile linalowapata watu wote. Lakini Mungu ni mwaminifu, Naye hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu. Pamoja na jaribu, Yeye atafanya pia njia ya kutokea, ili mweze kulistahimili.
Zaburi 36:5
BWANA, upendo Wako usiokoma unafika mpaka mbinguni, uaminifu Wako juu kama mawingu.
Waebrania 10:23
Tuushikilie ukiri wa tumaini letu bila kulegea hata kidogo, kwa kuwa yule aliyetoa ahadi hiyo ni mwaminifu.
Mada za Biblia
Tumaini · Rehema · Mwanzo mpya · Majaribu · Uraibu · Huruma · Vijana · Meza ya Bwana · Kanisa · Usafi wa kingono